Monday, April 30, 2007

Namna ya kufanya BAJIA ZA KUNDE


BAJIA ZA KUNDE: "BAJIA ZA KUNDE

VIPIMO

Kunde 1 � Vikombe
Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa � Kikombe
Baking soda � Kijiko cha chai
Masala 1 Kijiko cha chai
Maziwa 2 Vijiko vya supu
Chumvi 1 � Vijiko vya chai
Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu
Mafuta ya kukaangia

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

-Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi.
-Saga kwenye mashine (food processor) kisha mimina kwenye bakuli.
-Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi.
-Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja.
-Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bajia.
-Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive.
-Andaa bajia kwenye sahani na chatini uipendayo.

Imeeandaliwa na Alhidaaya"

No comments: